Jifunze Spanish

Learn Spanish in Kiswahili

Jifunze Spanish

Learn Spanish in Kiswahili

SOMO LA 3

Personal Pronouns katika Spanish

Maana ya Viwakilishi vya Nafsi

Viwakilishi vya nafsi ni maneno yanayotumika badala ya majina ya watu, wanyama, au vitu katika sentensi. Viwakilishi hivi hutumika kumaanisha mtendaji wa tendo katika sentensi, hivyo pia hujulikana kama Subject Personal Pronouns.

Orodha ya Viwakilishi vya Nafsi katika Spanish

Hapa kuna orodha kamili ya viwakilishi vya nafsi na maana zake kwa Kiswahili:

  • Yo – Mimi (I)

  • – Wewe (You – itumikayo kwa watu wako wa karibu, au wenye kuwazoea, na kwenye matumizi yasiyo ya kiofisi au kwa watu wenye vyeo juu yako. Mfano unaweza itumia kwa ndugu, rafiki, jamaa , wafanyakazi wenzako, n.k. Usiitumie kuwasiliana na mabosi zako kama haujazoeana nao au watu wakuu wengine kama viongozi wa serikali n.k.)

  • Usted – Wewe (You – itumikayo kwa watu wasio wa karibu au wale ambao haujazoeana nao sana. Hii inafaa sana kwa watu wa rika linalokuzidi ambao hamjazoeana, watu wenye vyeo ambao pia hamjazoeana.  )

  • Él – Yeye (He)

  • Ella – Yeye (She)

  • Nosotros – Sisi (We – wanaume au mchanganyiko wa jinsia zote)

  • Nosotras – Sisi (We – wanawake tu)

  • Ustedes – Ninyi (You – wingi, rasmi)

  • Ellos – Wao (They – wanaume au mchanganyiko wa jinsia zote)

Ellas – Wao (They – wanawake tu)

Personal pronouns za Spanish katika picha

Matumizi ya Kipekee ya Viwakilishi vya Nafsi katika Spanish

  1. Kutokuwepo kwa ulazima wa kutumia viwakilishi vya nafsi mara kwa mara
    Tofauti na Kiingereza ambapo ni lazima kutumia viwakilishi vya nafsi, katika Kihispania mara nyingi vinaachwa kwa sababu vitenzi huonyesha ni nafsi ipi inayofanya tendo. Mfano:

    • (Yo hablo español) (Mimi nazungumza Kihispania) → Inaweza kusemwa tu Hablo español bila “Yo,” kwani “hablo” tayari inaonyesha kuwa mtenda ni nafsi ya kwanza umoja (mimi). Hivyo kama ni unataka kusema Sisi huzungumza Spanish utasema tuu Hablamos español  badala ya Nosotros hablamos español, hiyo ni kwa sababu verb Hablamos tayari inaonyesha nani ni mtendaji, yaani sisi.

  2. Kutofautisha heshima katika mazungumzo
    Kihispania kina viwakilishi viwili vya kusema “wewe”:

    • hutumika kwa mazungumzo yasiyo rasmi, kama vile kati ya marafiki au familia.

    • Usted hutumiwa kwa heshima, kwa watu wazima, viongozi, au katika mazungumzo ya kibiashara. Kuwa makini katika kutumia Usted kwenye watu ambao ni wa karibu kwani inaweza tafsirika kama umekasirika au kama vile unajaribu kujitoa katika ukaribu na hao watu.
    • Kumbuka wakati baadhi ya wazungumzaji wa Spanish wanaweza kutumia Usted mahali ambapo wangepaswa kutumia Tú, hii wengi hufanya hivyo kwa mazoea lakini sio kwa kusudi kama la kujitoa kwenye ukaribu. Hivyo inabidi ujue mazingira ya hiyo usted ilivyotumika.
      Wakati mwingine usted inaweza tumika badala ya Tú kwa baadhi tuu ya nyakati kwenye mazungumzo na nyakati nyingine mzungumzaji akatumia Tú. Hiyo inawezakana ikawa ni pale anapotaka kuweka msisitizo wa heshima au kuonyesha ustaarabu.

  3. Zingatia kutambua jinsia kwenye Personal Pronouns za wingi:

    • Nosotros na Ellos hutumika kwa wanaume pekee au mchanganyiko wa wanaume na wanawake.

    • Nosotras na Ellas hutumika kwa wanawake pekee.

  4. Matumizi ya “Vosotros/Vosotras”

    • Hili ni neno la “ninyi” la kirafiki kwa wingi, lakini linatumika zaidi nchini Uhispania na si katika nchi nyingi za Amerika Kusini, ambako badala yake hutumika Ustedes kwa hali zote.



  1. Tofauti za lafudhi zinazoleta mkanganyiko

    • Tú vs Tu: ni personal pronoun yaani  “wewe,” lakini tu (bila mkato juu) ni kivumishi cha umiliki kinachomaanisha “yako.”

    • Él vs El: Él (yenye mkato) ni “yeye” wa kiume, lakini el (bila mkato) ni article “the” kwa majina ya kiume.

 

Hitimisho

Kujifunza viwakilishi vya nafsi katika Spanish ni hatua muhimu kwa yeyote anayetaka kuwa mahiri katika lugha hii. Kwa kuelewa matumizi yake na tofauti zake, unaweza kuzungumza Spanish kwa usahihi na kueleweka vyema!

EXERCISE

🔹 Maelekezo: Jibu maswali yafuatayo kulingana na uelewa wako wa viwakilishi vya nafsi (personal pronouns) katika Kihispania.

Sehemu ya 1: Chagua Jibu Sahihi (Multiple Choice)

  1. Ni ipi tafsiri sahihi ya “We” katika Kihispania ikiwa kikundi kina wanaume na wanawake?
    a) Nosotras
    b) Nosotros
    c) Ustedes
    d) Ellas

  2. Usted hutumika kwa:
    a) Mazungumzo yasiyo rasmi
    b) Marafiki wa karibu
    c) Watu wa heshima au rasmi
    d) Watoto wadogo

  3. Katika Kihispania, “They” linapotumika kwa kundi la wanawake pekee ni:
    a) Ellos
    b) Ellas
    c) Nosotros
    d) Vosotras

Sehemu ya 2: Jaza Pengo (Fill in the Blanks)

  1. (___) soy estudiante de español. (Mimi ni mwanafunzi wa Kihispania.)

  2. (___) son muy simpáticos. (Wao ni wachangamfu sana.)

¿De dónde eres (___)? (Wewe unatoka wapi? – isiyo rasmi)