Jifunze Spanish

Learn Spanish in Kiswahili

Jifunze Spanish

Learn Spanish in Kiswahili

SOMO LA 5

Verbs to Be katika Spanish

Verbs to be ni nini katika Spanish?

Ili uelewe vema verbs to be za Spanish, fanya kwanza revision ya verbs to be za English. Katika English, “verbs to be” ni vitenzi vinavyoeleza hali, sifa, au uwepo wa kitu au mtu. Mfano wake ni:

  • I am a teacher (Mimi ni mwalimu)
  • She is happy (Yeye ana furaha)
  • They are at home (Wao wako nyumbani)

Katika Kiswahili, tunatumia maneno kama ni, yuko, wapo, tupo, liko, zipo, nipo n.k.
Kwenye Spanish, verbs to be hufanya kazi hiyo hiyo niliyoitaja hapo juu utofauti tuu ni namna verbs to be zinavyobainishwa huku kwenye Spanish.
Mfano wa verbs to be katika Spanish ni soy na estoy ambazo zote hutumika kwa I yaani kumaanisha am ya English.
Mfano I am a teacher – Soy profesor.
I am happy – Estoy feliz.

Cha kujiuliza hapo ni kwa nini sasas tunazo AM mbili yaani soy na estoy zote zina maanisha AM yaani hutumika kwenye MIMI (I). Endelea kujifunza hapo chini.

Verbs to be za Spanish katika picha

Utofauti wa Verbs to be katika Spanish, Kiingereza, na Kiswahili

Tofauti kubwa kati ya Spanish, Kiingereza, na Kiswahili ni kwamba:

  • Kiswahili mara nyingi utakuta verb to be moja inaweza tumika kwa aina tofauti tofauti ya wahusika. Mfano Mimi ni Mwalimu. Wao ni walimu. Yeye ni mwalimu. Hapa unaona ni imetumika kwa aina tofauti ya wahusika yaani Mimi, Wao na Yeye zote zimetumia ni.
  • Kiingereza kina verb moja kuu ya “to be” ambayo hunyambulishwa kuendana na aina ya mhusika na tense. Mfano  (am, is, are, was, were).
  • Kwenye Spanish kuna aina mbili tofauti za verb to be: SER na ESTAR., na hizi verbs to be hunyambulishwa kuendana na mhusika na pia kuendana na tense. Kazi yako kubwa kwenye somo hili ni kwanza kujua utoauti kati ya SER na ESTAR na kisha ujue SER huwa vipi kwenye personal pronoun gani (mhusika) katika Simple Present Tense. Na pia ESTAR huwa vipi kwenye personal pronoun gani (mhusika) katika Simple Present Tense.

SER na ESTAR: Aina mbili za Verbs to be katika Kihispania

Katika Kihispania, kuna vitenzi viwili vya “to be” ambavyo hutumika katika hali tofauti:

  • SER – hutumika kwa hali za kudumu au sifa zisizobadilika haraka.
  • ESTAR – hutumika kwa hali za muda, mabadiliko, au mahali.

Kumbuka tunaposema SER na ESTAR tunamaanisha verbs mama ambazo ili ujue unaitumiaje SER au ESTAR inakupasa uzingatie MTENDAJI wa tendo. Yaani mfano SER ya mtendaji akiwa YO ni SOY, wakati SER ya mtendaji akiwa Nosotros (WE) itakua ni SOMOS.

Hivyo hivyo kwenye ESTAR tambua kwanza mtendaji ni nani, mfano kwa YO (I) estar  itakua ESTOY wakati kama ni Nosotros (WE) estar itakua itakua ESTAMOS.

Angalia picha hapa chini za majedwali ya jinsi SER na ESTAR zinavyobadilika kwa kila aina ya mtendaji wa tendo.

Wakati gani uitumie verb to be ya  SER

SER hutumika katika hali za kudumu, sifa, na kwenye utambulisho kama utakavyoona hapa chini:

Tumia SER kwa:
Utambulisho – Mimi ni mwalimu, yeye ni mwanafunzi.

  • Yo soy profesor (Mimi ni mwalimu)
  • Ella es estudiante (Yeye ni mwanafunzi)

Sifa zisizobadilika – Mfano rangi, taifa, jinsia.

  • El cielo es azul (Anga ni la bluu)
  • Soy tanzano/a (Mimi ni Mtanzania)

Tarehe, muda, siku

  • Hoy es lunes (Leo ni Jumatatu)
  • Son las tres de la tarde (Ni saa tisa mchana)

Uhusiano au umiliki

  • Este coche es mío (Gari hili ni langu)
  • Ella es mi hermana (Yeye ni dada yangu)

Kazi au dini

  • Él es doctor (Yeye ni daktari)
  • Somos cristianos (Sisi ni Wakristo)

Wakati gani uitumie verb to be ya  ESTAR

ESTAR hutumika katika hali zisizokua za kudumu, yaani hali za muda zenye ukomo fulani. Mfano kuchoka sio hali ya kudumu. Mtu hawezi kuwa amechoka tuu muda wote.
Pia ESTAR hutumika kwenye kutaja mahali.

    • Estoy estudiando (Ninajifunza)

       

      Tumia ESTAR kwa:
      Mahali/eneo – Watu au vitu vilipo

      • Estoy en casa (Nipo nyumbani)

         

      • El libro está en la mesa (Kitabu kiko mezani)

         

      Hali ya muda (mhemko, afya, hali ya hewa ya muda)

      • Estoy feliz (Nina furaha)

         

      • Estamos cansados (Tumechoka)

         

      • Está nublado (Kuna mawingu)

         

      Hali za muda za vitu au watu

      • La sopa está caliente (Supu ni moto)

         

      • El agua está fría (Maji ni baridi)

         

      Tendo linaloendelea (Present Continuous)

    • Estamos comiendo (Tunakula)

     

Hatua za kufuata katika kutumia verbs to be

Mfano 1: Chukulia kwa mfano tunataka kusema sentensi hii: Juma is a teacher (Juma ni Mwalimu)

Tutafuata hatua zifuatazo:

  1. Tambua mtendaji: Juan
  2. Tambua hali ya ujumbe: Kazi yake (ni mwalimu, jambo la kudumu. Hivyo hapa tunajua tunaenda kutumia SER)
  3. Linganisha na PERSONAL PRONOUN sahihi ili itusaidie kujua tutumie SER ipi. Kwakua ni JUMA basi personal pronoun yake ni : Él
  4. Chagua kitenzi cha ser kilichofaa. Kwa personal pronoun tuliyoitambua hapo juu Él, ukiangalia jedwali la SER unapata ni: Es

    Sentensi kamili:
    Juan es profesor. (Juma is a teacher.)

Hatua za kufuata katika kutumia verbs to be

Mfano 2: Chukulia kwa mfano tunataka kusema sentensi hii: Children are happy. (Watoto wana furaha)

Tutafuata hatua zifuatazo:

  1. Tambua mtendaji: Watoto
  2. Tambua hali ya ujumbe: Wana furaha.( Hali isiyo ya kudumu). Hivyo tunajua hapa verb to be ya ESTAR ndio itakayohusika.
  3. Linganisha na PERSONAL PRONOUN sahihi ili itusaidie kujua tutumie ESTAR ipi. Kwakua ni WATOTO basi personal pronoun yake ni : Ellos
  4. Chagua kitenzi cha estar kinachofaa. Kwa personal pronoun tuliyoitambua hapo juu ellos, ukiangalia jedwali la ESTAR unapata ni: Están

    Sentensi kamili:
    Niños están felices. (Children are happy)

Angalizo kuhusu Verbs to be katika tenses mbalimbali

✔ SER na ESTAR hubadilika kulingana na wakati (tense).
✔ Kwa sasa, kumbuka tu mifano kwenye jedwali na sentensi tulizotungani kwenye Simple Present Tense.
✔ Kwa wakati ujao, tutajifunza jinsi SER na ESTAR zinavyobadilika kwa wakati uliopita na wa baadaye.

Kwa sasa, cha muhimu ni kuelewa tofauti ya SER na ESTAR na jinsi ya kuzitumia!