SOMO LA 6
Adjectives katika Spanish
Maana ya Adjectives katika Spanish
Adjectives, kwa lugha ya Spanish “adjetivos,” ni maneno yanayotumika kuelezea au kufafanua sifa za nomino (majina ya vitu, watu, au sehemu). Kazi kuu za adjectives ni:
- Kuelezea sifa za nomino – Mfano: “El coche rojo” (Gari jekundu).
- Kutoa idadi au kiasi cha nomino – Mfano: “Tengo tres libros” (Nina vitabu vitatu).
- Kuelezea umiliki – Mfano: “Su casa es grande” (Nyumba yake ni kubwa).
Adjectives ni maneno ambayo mara nyingi utahitaji kuyatumia. Lakini kutumia adjectives katika Spanish kunakuhitaji ukumbuke kanuni za Gender tulizozisoma katika somo la 2, na pia uzingatie idadi ya noun ambayo inabeba adjective husika.
Katika somo hili utajifunza kanuni za msingi za matumiz ya Adjectives kwa ujumla. Hatutojikita kujua aina moja moja za Adjectives.
Kanuni za kutumia Adjectives katika Spanish

Usichanganye kati ya Adjectives na Pronouns
Adjectives na pronouns vina kazi tofauti katika sentensi:
- Adjectives hutumika kuelezea sifa za nomino moja kwa moja.
- Mfano: “Tengo un perro pequeño.” (Nina mbwa mdogo.)
- Pronouns hutumika badala ya nomino na mara nyingi huchukua nafasi yake.
- Mfano: “Tengo uno.” (Nina mmoja.) – hapa “uno” ni pronoun inayochukua nafasi ya “perro.”
- Adjectives hutumika kuelezea sifa za nomino moja kwa moja.
Kanuni mbili kuu za kutumia Adjectives katika Spanish
Katika Spanish, adjectives lazima zilingane na nomino katika:
- Jinsia (mwanaume/mwanamke)
Mfano: “El niño alto” (Mvulana mrefu) lakini “La niña alta” (Msichana mrefu).
Unaona katika sentensi hii sifa ya mrefu imeandikwa tofauti kwa kuangalia jinsia ya noun husika. Kwenye jinsi ya kiume tumetumia ALTO, kwenye jinsia ya kike tumetumia ALTA. - Idadi (umoja/wingi)
Mfano: “El perro negro” (Mbwa mweusi) lakini “Los perros negros” (Mbwa weusi).
Unaona katika sentensi hizo pale penye mbwa mmoja mweusi adjective ya NEGRO imekua katika umoja. Ila tulipokua na wingi wa mbwa yaani perros basi adjective ya NEGRO nayo ikapaswa kuwa katika wingi yaani NEGROS.
Mifano halisi ya kanuni za Adjectives
Salamu katika Spanish zinahitaji kutumia kanuni ya Spanish:
Mfano 1: Buenos Dias – Good morning
Kwa sababu DIA kwenye Spanish ni noun ambayo ni masculine, hivyo adjective yake ni masculine bueno.
Ila kwa sababu DIA ipo katika wingiyaani dias, ndio maana hiyo adjective ya bueno nayo imekua katika wingi yaani buenos.
Ila wasiozijua kanuni wengi hukosea kwa mfano kwa kusalimia buenas dias. Au Bueno dias.
Mfano 2: Buenas Tardes – Good afternoon
Kwa sababu TARDE kwenye Spanish ni noun ambayo ni feminine, hivyo adjective yake ni feminine buena.
Ila kwa sababu TARDE ipo katika wingi yaani TARDES, ndio maana hiyo adjective ya tarde nayo imekua katika wingi yaani tardes.
Ila wasiozijua kanuni wengi hukosea kwa mfano kwa kusalimia buenos tardes. Au Bueno tardes.
Mfano 3: Muchas Gracias – Thanks a lot (Thank you very much)
Kwa sababu GRACIA kwenye Spanish ni noun ambayo ni feminine, hivyo adjective yake ni feminine mucha.
Ila kwa sababu MUCHA ipo katika wingi yaani MUCHAS, ndio maana hiyo adjective ya mucha nayo imekua katika wingi yaani muchas.
Ila wasiozijua kanuni wengi hukosea kwa mfano kwa kusema mucho gracias. Au wengine husema mucha gracias.
Mpangilio wa Nomino na Adjective katika Spanish
Jambo lingine la msingi katika Katika Spanish ni kujua jinsi ya kupangilia kati ya Noun na Adjective ianze nini.
Kwa kawaida kwenye Spanish, huwa tunaanza kutaja nomino kisha adjectives kama ambavyo huwa tunafanya kwenye Kiswahili.
Mfano: A red car- Gari jekundu- Un coche rojo
Hapo Gari ni nomino, ikafuatiwa na adjective ya rojo yaani nyekundu.
Mfano 2: Un hombre feo – An ugly man (Mwanaume mbaya)
Hombre ni nomino, halafu feo ni adjective.
Umegundua kuwa mtindo huo wa kuanza na nomino kisha adjective ni kinyume cha vile ambavyo tumezoea kwenye English. Kwa sababu kwenye English huwa tunaanza na adjective kisha noun, mfano an ugly man. Hapo ugly ndio adjective, halafu man ndio noun.
Wakati gani adjective huanza kabla ya noun
Pamoja na ukweli kuwa mara nyingi kwenye Spanish noun huanza kisha adjective hufuata, kuna aina tatu za adjective ambazo zenyewe zikitumika mpangilio huwa tofauti na huo wa kawaida wa Spanish. Yaani zikitumika aina hizi tatu hapa chini, inakupasa uanze kwanza na adjective kisha noun.
Aina za adjectives ambazo huanza kabla ya noun ni zifuatazo:
- Possessive Adjectives (Adjectives zinazoonyesha umiliki):
Mifano:
Mi casa – Nyumba yangu).
Nuestro equipo – Timu yetu. - Demostrative Adjectives (Vivumishi vya kuonyesha):
Mifano:
Este libro – Kitabu hiki.
Esa casa-Nyumba hiyo - Adjetivos de cantidad (Vivumishi vya idadi):
Mifano
Muchos amigos – Marafiki wengi.
Cinco personas – Watu watano