SOMO LA 1
Jinsi ya Kutamka Maneno ya Spanish
Kuweza kutamka maneno ya Spanish kunawezesha na uelewa wako kuhusu herufi zinazotumika katika Spanish. Hivyo basi katika somo hili la kwanza utajifunza kuhusu herufi za Spanish zikiwa moja moja na pia zinavyotamkwa pale ambapo zinakua zimetumiwa kwenye maneno.
Hili ni somo muhimu sana kwa sababu katika somo hili ndio unaenda kujenga msingi wa sio tuu kuweza kutamka maneno ya Spanish, bali pia kuelewa watu wengine wametamka maneno gani.
Somo hili la 1 limegawanyika katika vipengele vitano ambavyo ni:
Fahamu herufi zinazotumika katika Spanish
Je, Ü na RR nazo ni herufi katika Spanish?
Jinsi ya kutamka herufi moja moja katika Spanish
Mifano ya matumizi ya kutamka herufi moja moja katika Spanih
Jinsi ya kutamka herufi za Spanish zikiwa katikati ya maneno
Fahamu namna maalum za kutamka RR na ü
Jipime kwa Mazoezi kadhaa ya kutamka maneno ya Spanish
Fahamu herufi zinazotumika katika Spanish
Herufi zinazotumika katika Spanish ni kama tuu zile za kwenye English isipokua kuna mbili ambazo zimeongeza. Herefu zinazoongeka katika Spanish tofauti na zile tulizozoea kwenye English ni
LL (ll)
Ñ (ñ).
Hivyo basi tukiziandika herufi zote za Spanish tunapata hivi:
A, B, C, CH, D, E, F, G, H, I, J, K, L, LL, M, N, Ñ, O, P, Q, R, S, T, U, V, W, X, Y, Z.
a, b, c, ch, d, e, f, g, h, i, j, k, l, ll, m, n, ñ, o, p, q, r, s, t, u, v, w, x, y, z
Je, Ü na RR nazo ni herufi katika Spanish?
Ingawaje huwa tunatumia Ü na RR katika kuunda maneno ye Spanish, hizo mbili hazichukuliwi kama ni herufi.
Ü na RR ni namna tuu ya kuelekeza namna maalum ya kutamka U na RR kuendana na ilipotumika. Tutajifunza baadae jinsi ya kuzitamka hizo Ü na RR.
Jinsi ya kutamka herufi moja moja katika Spanish
Herufi moja moja katika Spanish hutamkwa kama inavyoonekana katika maelezo hapa chini.
A: ah
B: beh
C: Se
CH: cheh
D: deh
E: eh
F: eh-feh
G: heh [Hapa h ya kwanza unaitamka]
H: ache .
I: ii
J: hota [Hapa h unaitamka]
K: kah
L: ele
LL: eje
M: eme
N: ene
Ñ: enye
O: oh
P: peh
Q: kuh
R: ere
S: ese
T: teh
U: u
V: ube
W: doble ube
X: ekis
Y: igriega
Z: seta au theta (nchini Hispania huitamka kama theta).
Mifano ya matumizi ya kutamka herufi moja moja katika Spanih
Ufahamu wa jinsi ya kutamka herufi moja moja katika Spanish ni muhimu haswa katika maeneo mawili:
Eneo la kwanza: Pale unapotaka kusema herufi moja moja zinazounda neno ( kwa English tunasema kuspell neno) utahitaji kutumia ujuzi wa kusema herufi moja moja. Kwa mfano ukitaka kuspell neno JOHN utasema hota- o-ache-ene
Mfano mwingine CASA utasema se-a-ese-a
Eneo la pili: Ni wakati unapotaka kutamka vifupi vya majina mbalimbali. Mfano Umoja wa Mataifa kifupi chake ni ONU, hivyo utatamka O-ENE-U.
Au kifupi PMA utatamka Pe-Eme-A
Jinsi ya kutamka herufi za Spanish zikiwa katikati ya maneno
Baadhi ya herufi za Spanish huwa na namna ya tofauti ya kutamkika zikitamkwa kama sehemu ya neno zima na sio herufi moja moja.
A: ah kama A kwenye ALMASI, mfano Casa ( nyumba) itasomeka KASA
B: beh kama B kwenye BAKULI mfano Bello(nzuri) itasomeka Bejo.
C: Kuna namna mbili za kuitamka C.
Kama C inafuatiwa na e au i, isomwe kama S kwenye SEHEMU mfano Cena (mlo wa usiku) utaisoma sena, Au mfano cine (sinema) utaisoma kama sine.
Kama C haijafutiwa na e au i, isomwe kama K kwenye KAKA. Mfano Casa (nyumba) itasomeka kasa. Mfano comida (chakula) utaitamka komida.
CH: cheh kama CH kwenye CHEMCHEM, mfano chico (kijana wa kiume) utaisoma chiko.
D: deh kama D kwenye DEKI mfano neno Dormir (kulala) litatamkwa dormir
E: eh kama E kwenye EMBE mfano kwenye neno hermano (kaka) utalitamka ermano.
F: eh-feh kama F kwenye EFREIM mfano fuego (moto) utalitamka fuego.
G: Kuna namna mbili za kuitamka G.
Kama H inafuatiwa na e au i, isomwe kama S kwenye HABARI mfano gente (mtu) utaisoma gente, Au mfano gigante (jitu) utaisoma kama higante.
Kama G haijafutiwa na e au i, isomwe kama G ya kawaida yaani kam vile G kwenye GARI. Mfano Gato (paka) itasomeka gato.
H: Kwenye Spanish herufi h huwa haitamkwi. Mfano kwenye salamu Hola utasema ola.
I: ii kama i kwenye IRINGA mfano ingles ( English).
J: Kwenye Spanish herufi J hutamkwa kama h mfano Jefe utaisomakama HEFE
K: Itamke tuu ka K ya kawaida, mfano neno Kiwi utalitamka kiwi.
L: ele itamke tuu kama L ya kawaida, mfano neno Luna utalisoma LUNA
LL: Kwenye Spanish L zikiwa mbili kama hivi LL utatamka J kama iliyopo kwenye JUA, Mfano: Llave(funguo) itatamkwa JAVE.
Kuna watumiaji wengine wa Spanish mfano watu wa Hispania kwenyewe ambao wao LL hutamkwa kama Y kwenye neno YESU. Hivyo LLave itatamkwa YAVE.
M: Hii itamkwe kama M ya kawaida mfano Madre(Mama) utasomeka tuu madre.
N: Hii itamkwe kama N ya kawaida mfano No (Hapana) utasomeka tuu no.
Ñ: Hii itamkwe kama vile kwenye nya, nye, nyi,nyo, nyu.Mfano SEÑORA, itasomeka senyora. Kwenye NIÑA utaisoma ninya.
O: Hii itamkwe kama O ya kawaida mfano Oso(Dubu) utasomeka tuu oso.
P: Hii itamkwe kama P ya kawaida mfano Pero(Lakini) utasomeka tuu pero.
Q: Kwenye Spanish Q hutamkwa kama K kwenye KWELI, ila siku zote Q hufuatana na U lakini hiyo U haisomwi , badala yake herufi inayoifuata U ndio hubeba tamko zima la neno husika. Mfano angalia neno QUIERO- itasomeka KIERO. Neno QUE, litasomeka KE.
R: Hii itamkwe kama R ya kawaida mfano Rápido(Haraka) itasomeka tuu Rapido
S: Hii itamkwe kama S ya kawaida mfano Sol(Jua) itasomeka tuu sol..
T: Hii itamkwe kama T ya kawaida mfano Tierra(Dunia au ardhi) itasomeka tuu tierra.
U: Hii itamkwe kama U ya kawaida mfano Uva(Zabibu) itasomeka tuu uba.
V: Hii itamkwe kama B mfano wa B ya kwenye BABA. Mfano Viento isomwe BYENTO.
W: Hii itamkwe kama W ya kawaida mfano Whisky(Whisky) itasomeka tuu wiski.
X:Hii itamkwe kama S ya kawaida mfano xilófono (xilophone) – itamkwe silofono
Y: Hii itamkwe kama J kwenye neno JUMA mfano wa apoyo(msaada) itatamkwa apojo.
Z: Z ina namna mbili ya kutamkika kutegemeana na aina ya wazungumzaji wa Spanish. Kuna wanaoitamka kama S kwenye neno Simba mfano Zapato itasomeka Sapato.
Ila kuna ambao huitamka kama th kwenye neno thamani. Hivyo kwao Zapato itatamkwa Thapato.
Fahamu namna maalum za kutamka RR na ü
- RR katika Spanish:
RR inatamkwa kwa mtetemo wa ulimi.
Mfano:- carro (gari)
- arriba (juu)
- Jinsi ya kutamka ü
Unapoiona herufi ü basi ichukulie kama W kwenye wewe. Hivyo mfano neno:
Pingüino (Penguin) utalisoma PingWIno.
Agüita (maji) utalisoma kama AgWIta
Bilingüe(Mtu mwenye kuongea lugha zaidi ya moja) utalisoma kama BilingWE
Agüero (Jina la mtu) utalitamka AgWero
Jipime kwa Mazoezi kadhaa ya kutamka maneno ya Spanish
ZOEZI
ZOEZI LA 1:Tamka maneno yafuatayo kwa usahihi
Real Madrid
Iker Casillas
Daniel Carvajal
Federico Valverde
James Rodríguez
ZOEZI 2: Isome story hii fupi kwa usahihi
La luna iluminó el viejo parque. Un gato negro saltó sobre un banco. De repente, un perro ladró desde la puerta. El gato corrió a un árbol, maullando con fuerza. Al final, ambos animales se miraron y decidieron dormir tranquilos bajo la luz suave.
ZOEZI 3: Soma story ifuatayo tena kwa usahihi
Bajo la lluvia, Javier, con su chaqueta y su yate en miniatura, vio un pingüino y una cigüeña extraña. Con vergüenza y ambigüedad, Wendy tocó un xilófono y gritó: “¡kilo de uvas para el zorro!” Todo ocurrió en la viña, quizá sin más explicación.
ZOEZI 4: Soma sentensi zifuatazo kwa usahihi , jitahidi usome kwanza taratibu halafu baadae uzisome haraka haraka.
Tres tristes tigres tragan trigo en un trigal, en tres tristes trastos.
Pepe Pecas pica papas con un pico, con un pico pica papas Pepe Pecas.
Parra tenía una perra y Guerra tenía una parra; Parra dijo a Guerra: “¿Por qué tienes tu perra debajo de mi parra?”
Cuando cuentes cuentos, cuenta cuántos cuentos cuentas, porque si no cuentas cuántos cuentos cuentas, nunca sabrás cuántos cuentos cuentas.
Compadre, cómpreme un coco. Compadre, no compro coco porque como poco coco como, poco coco compro.
El perro de San Roque no tiene rabo, porque Ramón Ramírez se lo ha cortado.
ZOEZI 5: Vifuatavyo ni vifupi vya asasi za kimataifa. Visome kama ambavyo huwa inatakiwa mtu kusoma herufi moja moja anapotaja kifupi cha jina fulani:
ONU (UN)
OMS (WHO)
FMI (IFM)
UE (UE)
OTAN (NATO)
OPEP (OPEC)