SOMO LA 2
Gender ya Maneno katika Spanish
Utangulizi
Katika lugha ya Spanish, maneno yana mgawanyiko wa jinsia (gender). Kila nomino huwa ya kike (femenino) au ya kiume (masculino). Hii ni tofauti na Kiswahili, ambacho hakina mgawanyiko wa jinsia kwenye nomino nyingi.
Ielewe kuwa jinsia tunayozungumzia hapa haina maana ya jinsia kimaumbile na hakuna maelezo ya kwanini nomino fulani ni ya kike au ya kiume.
Mfano, Nomino nyumba (casa) ni ya jinsia ya kike, wakati gari (carro) ni nomino ya kiume. Ukiniuliza kwanini sasa nyumba iwe ni ya kike , halafu gari ni la kiume hakuna jibu zaidi ya kukumbusha kuwa lugha ni sauti za nasibu zilizokubaliwa na watu wa jamii fulani zitumike kufanya mawasiliano.Hivyo basi kuna vitu vingi kwenye lugha fulani unaweza usielewe msingi wake haswa ni upi.
Ninachoweza kukuambia ni kuwa concept hii ya gender kwenye maneno ya Spanish ni muhimu sana kwani inafanya kazi kwa sehemu kubwa katika kuandika na kuzungumza lugha hii haswa pale unapotaka kutumia nouns(nomino), adjectives(vivumishi) na articles(vibainishi).
Wapi hujitokeza Concept ya gender kwenye Spanish
Dhana ya gender katika Kihispania huathiri vipengele mbalimbali vya lugha, ikiwa ni pamoja na:
- Kwenye Majina ya vitu, watu na wanyama:
Kuna kanuni zinazotuongoza kujua majina ya vitu, watu, mahali,hali na wanyama kuwa yapo kwenye kundi gani kama ni feminine au masculine. (mfano: “mesa” – meza, ni ya kike; “perro” – mbwa, ni ya kiume).
Utajifunza hizo kanuni hivi punde. - Viunganishi (articles):
Articles ni maneno ambayo hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino. Tunapotumia articles kwenye Spanish ni lazima article husika iendane na gender ya nomino inayoitolea taarifa ya ziada.(mfano: “el” kwa nomino za kiume na “la” kwa nomino za kike). - Vivumishi (adjectives):
Vivumishi ni maneno ambayo hutoa taarifa za zaidi kuhusu nomino mfano kusifia, idadi n.k. Aina mbalimbali za vivumishi kwenye Spanish huhitaji kuendana na nomino ambayo vivumishi hivyo vinavumisha.(mfano: “niño bonito” – mvulana mzuri, “niña bonita” – msichana mzuri) - Majina ya taaluma au kazi
Baadhi ya majina ya taaluma au kazi huhitaji uzingatie gender ya mhusika.
(mfano: “doctor” kwa daktari wa kiume, “doctora” kwa daktari wa kike, profesor kwa mwalimu wa kiume , halafu profesora kwa mwalimu wa kike)
Jinsi ya kutambua Nomino za Kike:
Kanuni za Jumla Kuhusu Nomino za Kike (Femenino)
Nomino nyingi za kike katika Kihispania zinaishia na herufi “-a”. Mfano:
- Casa (nyumba)
- Niña (msichana)
- Mesa (meza)
- Amiga (rafiki wa kike)
Aidha, nomino zinazoishia na “-ción” na “-dad” mara nyingi huwa za kike, kama:
- Nación (taifa)
- Universidad (chuo kikuu)
- Información (taarifa)
Nomino nyingi zinazoishia na “-z” pia huwa za kike. Mfano:
- La paz (amani)
- La luz (mwanga)
- La vez (mara)
Zingatia kichwa cha habari hapo juu kuwa hizo ni kanuni za jumla.Hii ni kwa sababu kuna wakati kanuni hizo za jumla hazifuatwi. Hii tunaita kuwepo kwa exceptions katika kutambua nomino za kike.
Hapo baadae utajifunza exceptions za majina ya feminine.
Yaani nomino ambazo zinaweza ishia na hivyo viashiria hapo juu lakini bado yasiwe ya kike. Mfano mzuri ni el día (siku)ambayo imeishia na A, lakini sio feminine.
Kanuni za Jumla Kuhusu Nomino za Kiume (Masculino)
Nomino nyingi za kiume katika Kihispania zinaishia na “-o”. Mfano:
- Perro (mbwa)
- Niño (mvulana)
- Libro (kitabu)
- Amigo (rafiki wa kiume)
Nomino zinazoishia na “-ma” mara nyingi huwa za kiume, kama:
- Problema (tatizo)
- Programa (mpango au programu)
- Sistema (mfumo)
Nomino zinazoishia na “-or” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- Color (rangi)
- Amor (upendo)
- Dolor (maumivu)
Nomino zinazoishia na “-aje” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- Viaje (safari)
- Mensaje (ujumbe)
- Paisaje (mandhari)
Nomino zinazoishia na “-án” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- Capitán (nahodha)
- Flan (aina ya keki au pudding)
- Pan (mkate)
Nomino zinazoishia na “-ón” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- Salón (ukumbi)
- Balón (mpira mkubwa)
- Corazón (moyo)
Nomino zinazoishia na “-l” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- Papel (karatasi)
- Hotel (hoteli)
- Sol (jua)
Nomino zinazoishia na “-r” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- Motor (injini)
- Dolor (maumivu)
- Valor (uthubutu)
Nomino zinazoishia na “-s” mara nyingi huwa za kiume. Mfano:
- País (nchi)
- Lunes (Jumatatu)
- Virus (virusi)
Pia, siku za wiki, namba, na lugha zote ni za kiume. Mfano:
- El lunes (Jumatatu)
- El tres (namba tatu)
- El español (Kihispania)
Hapo baadae utajifunza exceptions za majina ya masculine.
Yaani nomino ambazo zinaweza ishia na hivyo viashiria hapo juu lakini bado yasiwe ya kiume. Mfano mzuri ni la mano (mkono) ambayo imeishia na O, lakini sio masculine.
Exceptions za Feminine Nouns kwenye Spanish
Baadhi ya maneno yanayoishia na “-a” ni ya kiume licha ya kufuata kanuni ya kawaida. Mfano:
- El día (siku)
- El mapa (ramani)
- El planeta (sayari)
- El problema (tatizo)
Baadhi ya maneno yanayoishia na “-z” ni ya kiume licha ya kufuata kanuni ya kawaida. Mfano:
El lápiz – Penseli (pencil)
El arroz – Mchele (rice)
El pez – Samaki (fish)
El disfraz – Mavazi ya kuigiza (costume)
El matiz – Kivuli/Tofauti ndogo (nuance/shade)
El altavoz – Spika (loudspeaker)
El aprendiz – Mwanafunzi mwenye kujifunza (apprentice)
El capataz – Msimamizi wa kazi (foreman)
El haz – Fito la mwanga/kifungo (bundle/beam of light)
Baadhi ya maneno yanayoishia na d lakini sio feminine:
- El ataúd (jeneza) – coffin
- El césped (nyasi) – lawn/grass
- El ardid (hila) – trick/stratagem
- El almud (kipimo cha nafaka) – a grain measurement
- El sud (kusini) – south
Exceptions za Masculine Nouns kwenye Spanish
Baadhi ya nomino zinazoishia na “-o” ni za kike. Mfano:
- La mano (mkono)
- La radio (redio)
- La foto (picha, kutoka “fotografía”)
- La moto (pikipiki, kutoka “motocicleta”)
Nomino zinazomalizika na “-a” lakini ni za kiume:
- El día (siku)
- El mapa (ramani)
- El planeta (sayari)
- El sistema (mfumo)
- El problema (tatizo)
- El poema (shairi)
- El drama (drama)
- El cometa (nyota ya mwanga)
Nomino zinazomalizika na “-o” lakini ni za kike:
- La mano (mkono)
- La radio (redio)
- La foto (picha, kutoka “fotografía”)
- La moto (pikipiki, kutoka “motocicleta”)
Nomino za kiume lakini zinazomalizika na “-e”:
- El coche (gari)
- El puente (daraja)
- El hambre (njaa)
- El aire (hewa)
Nomino za kiume ambazo huonyesha mabadiliko ya maana:
- El capital (mtaji) – lakini La capital (mji mkuu)
- El frente (mbele, mstari wa vita) – lakini La frente (paji la uso)
- El corte (kata) – lakini La corte (jaji, utawala)
Gender katika Majina ya Kazi na Taaluma
Katika Kihispania, majina ya taaluma mara nyingi hubadilika kulingana na jinsia ya mtu anayefanya kazi hiyo. Mfano:
- Profesor (mwalimu wa kiume) – Profesora (mwalimu wa kike)
- Actor (mwigizaji wa kiume) – Actriz (mwigizaji wa kike)
- Doctor (daktari wa kiume) – Doctora (daktari wa kike)
- Abogado (wakili wa kiume) – Abogada (wakili wa kike)
Hata hivyo, kuna majina ya taaluma yasiyobadilika kwa jinsia, kama:
- Artista (msanii)
- Periodista (mwandishi wa habari)
- Dentista (daktari wa meno)
Mifano ya Matumizi ya Gender katika Maneno ya Kihispania
- Nomino na viunganishi:
- El coche es rápido. (Gari ni la haraka.)
- La casa es grande. (Nyumba ni kubwa.)
- Vivumishi vinavyobadilika kulingana na jinsia:
- Mi amigo es alto. (Rafiki yangu wa kiume ni mrefu.)
- Mi amiga es alta. (Rafiki yangu wa kike ni mrefu.)
- Majina ya taaluma:
- Mi madre es doctora. (Mama yangu ni daktari.)
- Mi padre es ingeniero. (Baba yangu ni mhandisi.)